Thursday 10 August 2017

UNAWEZA KUSAFIRI UKITUMIA NDEGE ISIYO NA RUBANI....?

Hilo ndilo swali mamilioni ya watu huenda wakajiuliza siku za usoni ikiwa wanataka kusafiri kwenda likizo kote duniani.

Tunaposogea karibu na kutumia magari yasiyokuwa na dereva, ambayo tayari yameingia barabarani katika baadhi ya miji nchini Marekani na pia kufanyiwa majaribio mjini London Uingereza, ndege zisizo na rubani huenda zikafuata.
Kampuni ya kuunda ndege ya Boeng inatarajia kufanyia majaribio ndege kama hizo ifikapo mwaka 2018.
Utafiti uliofanywa na kampuni inayohusiana na masuala ya kiuchumi UBS unaonyesha kuwa ndege hizo hazitapata umaarufu sana licha ya asilimia 54 ya watu 8000, kusema kwa huenda wakazitumia.
Moja ya suala linalozungumziwa zaidi kufuatia mpango huo ni usalama wa ndege hizo.
Wakati usafiri wa ndege ukitajwa kuwa mfumo ulio salama zaidi, ripoti ya UBS inasema ndege zisizokuwa na rubani zitaufanya usafiri huo kuwa salama zaidi.

UBS iligundua kuwa karibu asilimia 70 na 80 ya ajali za ndege husababishwa na makosa ya binadamu.

0 comments:

Post a Comment