Tuesday 1 August 2017

RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31

Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafanya kupata matibabu nchini Uingereza mwaka huu.

Lakini sasa rais wa miaka mingi wa Uganda Yoweri Museveni, amenukuliwa akisema kuwa hajawai kuwa mgonjwa kwa miaka 31.
"Mshasikia kuwa Museveni amekuwa mgonjwa au amelazwa hospitalini kwa miaka 31 iliyipota?" aliuliza Museveni.
"Hii ni kwa sababu ninafuata taratibu za kiafya ambazo zimenisaidia kuizuia baaadhi ya magonjwa kama haya, mengi ya magonjwa hata yanazuiwa."
Baadhi ya marais ambao pia wamesafiri ng'ambo kupata matibabu tangu mwaka uliopita ni pamoja na marais wa Angola, Zimbabwe, Benin na Algeria.


Rais wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 amekosolewa na wapinzani kwa kuiongoza nchi "kutoka hospitalini" baada ya kufanya ziara ya tatu nchini humo kupata matibabu mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment