Tuesday, 29 August 2017

HUYU NI MTU ANAYEFUNZA KOMPYUTA KUTAMBUA HARUFU…

Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.

Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya vilipuzi na unaweza kutumiwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, alisema.
Vilevile kifaa hicho kilicho na ukubwa wa modem na kupewa jina Koniku Kore kinaweza kuwa ubongo wa roboti za siku za usoni.
Kampuni kubwa za kiteknolojia, ikiwemo Google hadi Micrososft ziko katika harakti ya kutengeza roboti inayoweza kuwa na akili ya mwanadamu.
Huku Kompyuta zikiwa bora kushinda mwanadamu katika kutatua hesabu ngumu, kuna majukumu mengi ambayo yanaweza kufanywa na ubongo wa mwanadamu ikiwemo kuifunza kompyuta kutambua harufu.
Bwana Agabi analenga kubadili baiolojia ya uhandisi ambayo tayari imetimiza uvumbuzi huo.''Biolojia ni Teknolojia''.
Kazi yetu kuu ni kujaribu kuiga ubongo.
Alizindua kifaa hicho cha koniku yapata mwaka mmoja uliopita na amefanikiwa kuchangisha dola milioni moja kama ufadhili na anasema kuwa kifaa hicho kimempatia dola milioni 10 katika mikataba na kampuni za usalama.
Koniku Kore ni kifaa kilichotengezwa kwa kutumia neva na silicon ambacho kina sensa ambazo zinaweza kutambua harufu.

Unaweza kuzipa neva hizo maelezo ya ni unachotaka zifanye ambapo upande wetu tunaziambia kutoa seli zinazoweza kutambua harufu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment