Wakati matokeo ya tafiti mbalimbali
yanaendelea kutolewa kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya, matokeo ya utafiti mpya
uliofanywa na Infotrak, unaonesha mgombea wa kambi ya upinzani ya NASA Raila
Odinga angepata ushindi mwembamba dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kama uchaguzi
ungefanyika jana.
Matokeo hayo ya utafiti yanaonesha kuwa
Raila alipata asilima 49 dhidi ya Kenyatta,ambaye alipata asilimia 48.
Mgombea wa Tunza Abduba Dida angepata
asilimia 0.3 na Ekuru Aukot angepata asilimia 0.1 ya kura zote,huku asilimia 2
wakisema bado hawajafanya maamuzi.
Akisoma
matokeo ya tafiti hizo jijini Nairobi Afisa Mtendaji Mkuu wa Infotrak Angela
Ambitho, amesema utafiti huo ulifanyika kwa kuchukua sampuli kutoka kwenye
daftari la wapiga kura la Tume Huru ya Uchaguzi IEBC.
Utafiti huo uliowahusisha wapiga kura elfu
5, ulionesha kuwa Raila anaongoza zaidi katika maeneo ya Pwani, Mashariki, Magharibi,
Nyanza na Nairobi, wakati Kenyatta akiongoza maeneo ya Rift Valley, Kusini
Mashariki na Mikoa ya Kati.
Kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu
Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi unaotajwa kuwa wa ushindani mkubwa kuwahi kutokea
katika historia ya nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment