Tuesday, 1 August 2017

MWIZI AKUTWA AMELEWA NDANI YA NYUMBA ALIOVUNJA….

Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia kwa wizi, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.


Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na kuingia nyumbani humo mjini Esperence, magharibi mwa Australia siku ya Ijumaa.
Alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho, kulingana na sajenti Richard Moore kutoka polisi ya Esperence.
Mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani na kumpata mwizi huyo amelala kitandani mwake.
Ndipo alipotoka nje na kuwapigia simu polisi ambao waliwasili na kumkamata mshtakiwa.

Mtu huyo alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana amelewa chakari alisema sajenti Moore wa eneo hilo la Esperence.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment