Thursday, 17 August 2017

PETE ILIOPOTEA KWA MIAKA 13 YAPATIKANA KATIKA KAROTI….

Mwanamke mmoja wa Canada alipata karoti ya ziada na pete ya almasi baada ya kupatikana katika shamba lake la mboga miaka 13 baada ya kuipoteza.

Mary Grams mwenye umri wa miaka 84 alipata shida alipopoteza pete hiyo wakati akipalilia shamba la familia mjini Alberta 2004.
Lakini alifanya kupotea kwa pete hiyo kuwa siri kwa takriban miaka 13.
Siku ya Jumatatu mkwe wake aligundua siri hiyo na pete hiyo baada ya kuvuna karoti moja.
Karoti hiyo ilikuwa imemea kupitia pete hiyo.
Aliamua kutomwambia mumewe wakati alipoipoteza, kwa kuona aibu, lakini alimwambia mwanawe.
Alienda kununua pete iliofanana na aliyopoteza na kuvaa na kuendelea kuishi kama ambaye hakuna kilichotokea.
''Pengine nilifanya makosa lakini mara nyengine unachanganyikiwa'', alisema.
Lakini hakuna aliyekuwa na busara hadi wiki hii wakati mkwewe Collen Daley kuamua kwamba alihitaji karoti kwa chakula cha jioni.
Bi Daley ambaye sasa anaishi katika shamba hilo ambapo bi Grams alikuwa akiishi alienda kuvuna katika shamba hilo.
Aliona pete hiyo wakati alipokuwa akiosha karoti moja kubwa.
Mwanawe alijua pete hiyo ilikuwa ya nani na kumuita mamake.
Akikumbuka, bi Grams alisema kuwa anatamani angekuwa amemwambia mumewe ambaye alifariki miaka mitano iliopita.
''Alikuwa na mzaha mwingi'', alisema ''na angeona kisa hiki chote cha kufurahisha''.
Na baada ya kuipata sasa anasema kuwa atakuwa na tahadhari.
''Ninapoenda nje nitaiweka katika eneo salama. Na hivyo ndio nilifaa kufanya'',alisema.
Hii sio mara ya kwanza mtu amepata pete ya almasi katika karoti.
Mwaka 2011, mwanamke mmoja wa Sweden alipata pete yake miaka 16 baada ya kuipoteza.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment