Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la
maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani.
Hii ni kwa mujibu wa
watafiti nchini Japan.
Utafiti huu uliowahusisha watu elfu 37,000, ulichapisha taarifa
kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara
kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.
Hata hivyo watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache
ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.
Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini
Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapaswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi
kuliko kuchunga nywele zao.
Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume .
Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80
ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.
Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa
miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na
maradhi ya moyo.
Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano
na maradhi ya moyo.
Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia
ya familia.
Daktari Tomohide Yamada wa chuo kikuu cha Tokyo,amesema kuwa
walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo.
Amesema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa
kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo
Aidha amesema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa
wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.
Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini
Uingereza.
Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya
moyo.
Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo
pale inapoziba.
Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti
huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.
0 comments:
Post a Comment