Wednesday 27 February 2013

Mazoezi makali yanaongezea umri?..

Wewe ni mkimbiaji au muinua vyuma? Wakimbia katika mbio za masafa marefu au katika mashindano ya michezo mitatu tofauti - triathlon? Ni mazoezi yapi ambayo unaweza kufanya ikiwa unataka kujiongezea umri? Je, ni vyema zaidi kufanya mazoezi mafupi na makali, au marefu zaidi lakini ya taratibu? Kwa mujibu wa Daktari Jamie Timmons, Profesa wa masomo ya bayologia ya uzee katika Chuo Kikuu cha Birmingham, dakika tatu za mazoezi makali kila juma kwa majuma manne kunaweza kukaboresha, kwa kiwango kikubwa, afya ya mtu. Mazoezi haya makali yanaweza kusaidia moyo na mapafu yako kusambaza hewa mwilini vyema zaidi. Pia yanaboresha ifanyavyokazi insulini, ambayo inaondoa sukari mwilini na kudhibiti mafuta. Nao utafiti wa Daktari Stuart Gray wa Chuo Kikuu cha Aberdeen unadhihirisha kwamba mazoezi makali na mafupi, kama kukimbia kwa kasi kwa masafa mafupi, au kuendesha baiskeli kwa sekunde 30 tu, kunaufanya mwili uondoe mafuta kutoka kwenye damu haraka zaidi kuliko kufanya mazoezi ya wastani, kama kutembea harakaharaka. Kuondolewa kwa mafuta kutoka kwenye damu ni muhimu kwa vile kunapunguza uwezekano wa kukumbwa na tukio la mshtuko wa moyo.

0 comments:

Post a Comment