Monday, 25 January 2016

BARIDI KALI YAUA WATU 50….

Watu zaidi ya 50 wamefariki nchini Taiwan, kutokana na wimbi la baridi kali ambalo limeathiri maeneo ya Asia Mashariki.

Watalii zaidi ya elfu 60 pia wamekwama Korea Kusini, kutokana na karidi hiyo.
Vyombo vya habari nchini Taiwan vinasema kuwa, vifo hivyo vimetokana na kushuka sana kwa kiwango cha joto mwilini na wengine wakafariki kutokana na maradhi ya moyo.
Hii ni baada ya viwango vya joto kushuka ghafla wikendi.
Hayo yakijiri theluji nyingi imesababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege katika kisiwa cha Jeju nchini Korea Kusini, ambacho ni maarufu sana kwa watalii.
Wimbi hilo la baridi limeathiri sana Hong Kong, Uchina kusini na Japan.
Walioathirika zaidi Taiwan ni wazee wanaoishi maeneo ya kaskazini kama vile Taipei, Kaohsiung na Taoyuan.
Katika baadhi ya maeneo ya Taiwan viwango vya joto vilishuka hadi nyuzi 4C siku ya Jumapili.

Hong Kong hali ilikuwa mbaya zaidi, baadhi ya maeneo yakishuhudia vipimo vya joto vya nyuzi 3C, kikiwa ndicho kiwango cha chini zaidi kushuhudiwa eneo hilo katika kipindi cha miaka 60.

Related Posts:

  • Usikose kusoma nakala yako ya gazeti la TABIBU leo alhamisi kwa bei ya sh.500/= tu                                       &nbs… Read More
  • Mwanajeshi ashambuliwa na duma akipiga picha… Jeshi la wanahewa la Afrika Kusini limesema kuwa,duma wawili ambao hufugwa kwenye kambi ya jeshi hilo ili kufukuza wanyama wengine kwenye njia ambayo hutumiwa na ndege kupaa, wamemshambulia afisa wa jeshi. Msemaji wa j… Read More
  • Usikose kusoma nakala ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi.                                               &… Read More
  • Hili ndilo Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli Kabala ya kutaja majina ya mawazairi waliopo katika baraza lake, Rais Magufuli ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri hao, zielekezwe kwajili ya matumizi mengine.   Baraza hilo jipy… Read More
  • Malaysia yatafuta mmiliki wa ndege zilizoachwa uwanjani… Serikali ya Malaysia imeweka tangazo magazetini,ikitafuta mmiliki wa ndege tatu aina ya Boeing 747 ambazo zimeachwa katika uwanja wa ndege Kuala Lumpur. Tangazo hilo lililotolewa na mamlaka ya viwanja vya ndege,limeonya … Read More

0 comments:

Post a Comment