Tuesday 26 January 2016

VIBOKO NI MARUFUKU AFRIKA KUSINI..!!!

Kanisa moja nchini Africa Kusini lilikiuka katiba kwa kuhimiza watoto kuchapwa viboko, imesema tume ya haki za binadamu nchini humo.

Haikubaliki kanisa la Joshua Generation kuwahimiza waumini wake kuwaadhibu watoto wao kwa kuwachapa viboko hata kama inaambatana na mafunzo ya kidini.
Tume hiyo ya kupigania haki za kibinadamu ya Afrika Kusini, inasema kuwachapa viboko watoto kama njia ya kuwadhibu kunakiuka haki zao .
Msemaji wa kanisa hilo Nadene Badenhorst, amesema kanisa hilo litakata rufaa dhidi ya uamuzi.
Anasema sheria hiyo itasababisha kuzorota kwa viwango vya adabu katika jamii mbali na huo kwani utasababisha kuwepo kwa watoto watundu.

Badenhorst ''iwapo mzazi hataweza kumuadhibu mtoto nani atawajibikia utundu na kuzorota kwa maadili ya kijamii, shirika la habari la Eyewitness la Afrika Kusini liliripoti

0 comments:

Post a Comment