Monday 4 January 2016

Kikundi chenye ‘shortgun’ chatikisa Moshi…

Hofu imewakumba wakazi wa Moshi mjini, baada ya kudaiwa kuibuka kwa kikundi kinachoua watu kwa bunduki aina ya shortgun na kupora fedha na mali.

Taarifa zinadai miongoni mwa washirika wa kikundi hicho ni kijana ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, lakini akatoka Julai mwaka jana baada ya kushinda rufaa yake Mahakama Kuu.
Hata hivyo taarifa nyingine zinadai huenda ni vikundi viwili tofauti, kimoja kikivamia wafanyabiashara na kupora fedha na kingine kikionekana kufanya mauaji baada ya kukodiwa.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makala, amesema jana kuwa kuwa siku za kikundi hicho zinahesabika na kitatiwa mbaroni.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro Ramadhan Mungi, amesema wanaendelea na msako wa kuwakamata wahusika wote.

Kamanda Mungi amewataka wenyeviti wa mitaa, wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na raia wema, kutoa taarifa za siri kwake kwa vile mipango ya kihalifu mingine hupangwa ndani ya Jamii.

0 comments:

Post a Comment