Jimbo lenye wakazi wengi zaidi nchini Pakistan la Punjab, limeamuru kufungwa
kwa shule zote kwa siku tano na kuwataka wanafunzi wapatao milioni 22.5 kubakia nyumbani.
Hatua hiyo haihusiani na hofu ya usalama baada ya watu wenye silaha kukishambulia chuo kikuu nchini humo, bali ni kutokana na hali mbaya ya baridi kali.
Waziri wa elimu wa jimbo hilo Rana Mash hood, amesema idadi kubwa ya wanafunzi wanapatwa na mafua na kichomi katika kipindi cha baridi kali.
Hii ni kutokana na nyuzi joto hushuka na kufikia nyuzi joto 4 katika mji mkuu Lahore, na ukosefu mkubwa wa gesi husababisha shule kushindwa kuweka mazingira ya joto.
Waziri huyo ameliambia shirika la habari la reuters kwamba, siku mbili ilizopita wazazi walilalamika juu ya hali mbaya ya hewa, pamoja na magonjwa kwa watoto wao.
0 comments:
Post a Comment