Watu katika eneo
la Uhispania kaskazini mwa bara la Afrika la Melilla, walilazimika kukimbilia
mitaani baada ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.3 kipimo cha
Richter,lililoyaharibu majengo yakiwemo makao makuu ya serikali.
Rais wa serikali
ya Melilla ambayo ni milki ya Uhispania Juan Jose Imroda, amesema hakuna hasara ya
binaadamu ilioripotiwa.
Televisheni ya
Uhispania ilionyesha picha za majengo yalioporomoka na watu wakikimbia mitaani,
wengine wakiwa bado wamevaa nguo za kulalia.
Melilla yenye wakaazi elfu
85 imezungukwa na Morocco na bahari ya Mediterania.
0 comments:
Post a Comment