Monday 11 January 2016

Wavaa vimini wacharazwa bakora..!!


Viongozi wa Kitongoji cha Kasalazi kilichoko katika Kijiji cha Kanyara wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, wanadaiwa kuwachapa fimbo hadharani wanawake wanaovaa nguo fupi na za kubana zinazoonyesha baadhi ya sehemu zao za siri.

Pia viongozi hao wanadaiwa kuwatoza faini ya Shilingi elfu  20,wanawake wanaokutwa na nguo hizo kama njia ya kuwafanya wasiendelee kuvaa nguo hizo.
Mmoja wa wasichana waliowahi kuchapwa na viongozi hao aliyejitambulisha kwa jina la Juliana Mafuru, alichapwa fimbo baada ya kufika kijijini hapo kwa lengo la kununua dagaa.
Amesema cha kushangaza ni kwamba, baada ya kufika katika kitongoji hicho, mgambo walimkamata na kumchalaza bakora mbele za watu nje ya boti aliyokuwa amemepanda.
Nao wakazi wa kijiji hicho Lafael Bitulo na Mariamu Chacha, wamesema mwenyekiti wa kitongiji hicho na katibu wake, ndiyo vinara wa tabia hiyo kwa kuwa wamekuwa wakinufaika nayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Andrea Mkama, amekiri kuwachapa fimbo wanawake wanaovaa nguo fupi na zinazobana kwa mavazi wanayovaa ni ya udharirishaji.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kanyara Lazoro Mgonzo, amethibitisha wanawake kuchapwa fimbo ingawa amesema ni kitendo cha udharirishaji.

Mkuu wa Wilaya Sengerema Zainabu Terack, alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema hana taarifa ingawa aliahidi kulifuatilia.

0 comments:

Post a Comment