Thursday 14 January 2016

Al Jazeera yafunga runinga Marekani…

Shirika la habari la Al Jazeera limefunga matangazo ya Televisheni nchini Marekani ikiwa ni chini ya miaka mitatu tangu kuzindua huduma zake nchini humo.

Al Jazeera imesema kuwa imelazimika kufunga matangazo yake kutokana na ugumu wa mazingira ya soko la televisheni nchini humo.
Shirika hilo lenye makao makuu yake Qatar limesema kuwa badala yake linaimarisha na kupanua huduma ya kimtandao katika maeneo ambayo yanaendesha mfumo huo kwa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Al Jazeera imeshindwa kuwavutia watazamaji wa kutosha nchini Marekani ili kuweza kujitengenezea faida.

0 comments:

Post a Comment