Thursday, 14 January 2016

Marekani kuwalinda simba wa barani Africa..!!



Simba walioko barani Afrika watalindwa zaidi mwaka huu, kufuatia kuuawa kwa simba maarufu
aliyejulikana kama Cecil nchini Zimbabwe na Daktari kutoka Marekani mwaka wa 2015.
Marekani imeweka sheria kali zaidi kudhibiti uagizaji wa vito, vilivyotengenezwa na mabaki ya simba waliouwa.
Sheria hiyo itaanza kutetekelezwa tarehe 22 mwezi huu, na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuagiza vito vilivyotengenezwa kutoka kwa wanyama pori.
Aidha taasisi inayosimamia na kuthibiti uuzaji wa vito vilivyotengenezwa na mabaki ya wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia, pia inatarajiwa kuimarisha hadhi ya Simba duniani.
Idadi ya Simba barani Afrika imepungua kwa asilimia hamsini tangu miaka ya tisini.
Jamii ya kimataifa iliangazia zaidi hatma ya Simba barani Afrika, baada ya Daktari mmoja Walter Palmer raia wa Marekani kumuua Simba Cecil katika mbuga ya wanyama ya Hungwe nchini Zimbabwe Julai mwaka uliopita.
Disemba mwaka wa uliopita shirika la wanyama pori nchini Marekani, lilitangaza kuwa simba wote kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika,watawekwa katika kitengo maalum cha wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

Tangazo hilo litakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa itakuwa vigumu kwa watalii na wawindaji kuagiza vichwa vya simba, kucha na ngozi kutoka maeneo hayo.

Related Posts:

  • Kizee chauawa kwa kudaiwa mchawi,India……. Wanyama pia hutumiwa katika ushirikina Bibi kizee mmoja amenyongwa hadi kufa na wanakijiji wenzake, kwa tuhuma za ushirikina, kaskazini mashariki mwa India. Polisi katika jimbo la Assam wamesema mwanamke huyo mwenye umr… Read More
  • Picha ya kwanza kutoka sayari ya Pluto…… Picha ya kwanza inaonyesha kwa undani sayari ya Pluto ilivyo imeonyeshwa kwa mara ya kwanza duniani. Picha hiyo imepigwa na chombo kisicho na binadamu kilichotumwa kwenye safari hiyo ambacho kilisafiri umbali wa kilometa… Read More
  • Umri wa kuolewa Uhispania ni miaka 16… Uhispania imepandisha umri unaoruhusiwa kwa wasichana kuolewa hadi kumi na sita. Hadi sasa wasichana nchini humo wangeruhusiwa kuolewa wakiwa na miaka kumi na nne bora tu wapate ruhusa ya jaji. Sheria hiyo mpya sasa i… Read More
  • Je wajua kuna tamasha la mbu Urusi…..? Watu wengi wanawachukia, lakini mbu sasa husherekewa kwa tamasha la kipekee katika mji mmoja huko nchini Urusi. Pengine la ajabu zaidi kwenye hafla hiyo ni kuwepo kwa mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi, ambap… Read More
  • George HW Bush avunjika shingo.......... Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush amelazwa hospitalini baada ya kuvunjika mfupa wa shingoni alipoanguka nyumbani kwake huko Maine. Msemaji wake amesema kuwa kwa sasa yuko katika hali nzuri na kwamba kulazwa kwake h… Read More

0 comments:

Post a Comment