Tuesday 25 September 2012

USOMAJI WA VITABU WAPUNGUA KWA SABABU YA MITANDAO YA KIJAMII???

Nimejikuta natafakari jambo hili na kuingia kwenye marumbano makubwa na serikali ya kichwa changu hasa nikiangalia hali halisi tunayoishi sasa. Mapinduzi ya kompyuta yamebadilisha sana maisha. Enzi zile hata ukipewa assignment darasani unakimbia maktaba kutafuta kitabu. Siku hizi mambo yamebadilika. Hata assignment inapotolewa wanafunzi wanakimbilia kwenye Internet maana vitu vinapatikana kwa urahisi zaidi. Najiuliza kwa staili hii kweli watu hasa walio na access ya Internet wastani wao wa kusoma vitabu ukoje? Ripoti moja ilishawahi kuonyesha kuwa ujio wa smartphone na mitandao ya kijamii inawashawishi sana watoto wasome vitabu. Ilinipa wakati mgumu sana kuitafakari ripoti hii iliyotolewa kutokana na utafiti mmoja nchini Marekani. Nikiangalia mazingira yetu inanipa wakati mgumu sana kuamini jambo hilo. Naona kama vile uwezo na hamu ya watu kusoma vitabu unapungua zaidi wakipendelea kuingia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusoma hiki na kile! Hii ndiyo Teknolojia Yetu…

0 comments:

Post a Comment