Monday, 10 September 2012

Faida za Tende Mwilini Mwako.

Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin,protini,wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana Mwezi wa Ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Ebu zijue faida zake……. Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni, na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Baadhi ya faida zake mwilini ni kama ifuatavyo: 1-Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende,husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo. 2-Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu,ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki,moyo wako utakuwa imara. 3-Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali,kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi. 4-Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba,wakati mwanamke anapokaribia kujifungua,hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua. 5-Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha,kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema. 6-Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini. 7-Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee,na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua. 8-Kutokana na madini ya chuma kwenye tende,watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni. 9-Vitamin B1 na B2 zilizopo kwenye tende,husaidia kuyapa nguvu maini. 10-Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.

Related Posts:

  • NYAMA IKAE SAA NANE KABLA YA KUPIKWA............. Nyama nyekundu ni kitoweo kitokanacho na wanyama. Mbali na wanyama wa porini, watu wengi hupata nyama hiyo kutokana na kuchinja wanyama wafugawao kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia. Nyama nyekundu hutakiwa kuandaliwa… Read More
  • ASILIMIA KUBWA YA WANAUME HAWANA NGUVU ZA KIUME…. Utafiti wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) umebaini kuwa asilimia 33 ya wanaume 672 mkoani Dar  es salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume. Hayo yamezungumzwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya… Read More
  • VIDEO: JOH MAKINI FT DAVIDO-KATA LETA Rapa kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amekuja na video yake mpya iitwayo Kata Leta ambayo amemshirikisha Staa kutoka Nigeria, Davido. Tazama video yenyewe hapa chini. … Read More
  • ADAKWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI MAABARA.. Mwalimu wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St Therese mjini Lusaka ambaye alidakwa akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara ya shule hiyo amesimamishwa kazi akisubiri hatua za kinidhamu dh… Read More
  • MAMAKE ZARI HASSAN AAGA DUNIA….. Zari Hassan anaomboleza kifo cha mamake miezi miwili tu baada ya kumzika aliyekuwa mumewe Ivan Ssemwanga. Kulingana na gazeti la daily nation nchini Kenya. Mfanyibiashara huyo ambaye ni mke wa msanii wa bongo Diamond Pl… Read More

0 comments:

Post a Comment