Kitunguu swaumu
ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaaluma, huitwa allium sativum. Jamii hii
ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na
Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo
katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye
vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi
mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika
mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani
yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuepua mboga yako toka
katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake.
Lakini ili upate faida zaidi za
kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa
kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje 6
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo
katika hewa kwa dakika 10
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda
kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo
lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza
harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo
kwenye mtindi.Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo
utakuwa mbali na kuuguwauguwa.
Haya ni baadhi ya magonjwa
yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
Huondoa sumu mwilini, Husafisha tumbo, Huyeyusha mafuta mwilini
(Cholestrol), Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I, Hutibu amoeba, minyoo na
Bakteria wengine, Huzuia kuhara damu (Dysentry), Huondoa Gesi tumboni, Hutibu
msokoto wa tumbo, Hutibu Typhoid, Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi, Hutibu
mafua na malaria, Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu, Huongeza SANA
nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume), Hutibu
maumivu ya kichwa, Hutibu kizunguzungu, Hutibu shinikizo la juu la damu, Huzuia
saratani/kansa, Hutibu maumivu ya jongo/gout, Huuongezea nguvu mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula, Huongeza hamu ya kula, Huzuia damu kuganda, Husaidia
kutibu kisukari, Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni
moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa
msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
Sifa kuu za kitunguu swaumu ni
kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni pamoja kuwa na viasili kadhaa
(ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji
unatokana na mambo yafuatayo;
a. Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu
(vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen
sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
b. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha
kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
c. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin
ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina
mbalimbali.
d. Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide
ambayo hutolewa baada ya kuvila.
KUMBUKA :
Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie vitunguu swaumu kwani vinaweza
kusababisha madhara.
0 comments:
Post a Comment