Polisi wakishirikiana na maafisa wa wanyamapori nchini Afrika Kusini
wanawawinda simba watatu ambao wametoroka kutoka kwenye mbuga ya taifa ya
Kruger.
Kutoroka kwa simba hao
kumezua wasiwasi kwamba huenda wakawashambulia watu au mifugo.
Haijabainika ni vipi
simba hao walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mbuga hiyo maarufu, lakini polisi
wamewahimiza raia kuwa macho hasa katika maeneo yanayokaribia mpaka wa nchi
hiyo na Msumbiji.
Msemaji wa polisi
Leonard Hlathi alinukuliwa na eNCA akisema: "Wananchi wanafaa kuwa macho.
Simba hao bado hawajakamatwa na wanasalia kuwa hatari kwa sababu barabara hiyo
hutumiwa na watu wengi. Watu wanaopitia barabara hiyo wakiwa na magari wanaweza
kuyaegesha kando ya barabara kwenda haja ndogo, jambo ambalo linaweza kuwaweka
hatarini."
Taarifa ya Shirika la
Mbuga za Taifa Afrika Kusini imesema wakazi wa eneo la Komatipoort na maeneo ya
karibu katika jimbo la Mpumalanga ndio wanaofaa kutahadhari.
Msemaji wa shirika
hilo Rey Thakhuli anaripotiwa kuwaona simba hao katika makutano ya barabara ya
N4 / Mananga Jumatatu asubuhi eneo la Komatipoort.
"Inaaminika simba
hao walitoweka na kuingia kwenye mashamba ya miwa kilomita nne kutoka kwa mbuga
ya Kruger," amesema.
"Tunawahimiza
watu wajiepushe kupiga picha wanyama hao watakapowaona kwani ni wanyama
hatari…na inaaminika tayari wamemuua ng'ombe mmoja," amesema Thakhuli.
Mwaka uliopita, simba
waliripotiwa kutoweka kutoka kwenye Mbuga ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya na
kuingia maeneo ya makazi.
Hakuna aliyeshambuliwa
na wanyama hao.
0 comments:
Post a Comment