Wafungwa 17 wameuawa
kwa kupigwa risasi na askari gereza walipokuwa katika harakati za kutoroka jela
huko Papua New Guinea, nchi ndogo iliyoko kusini magharibi mwa bahari ya
Pacific.
Ingawaje tukio hilo
lilitokea Ijumaa iliyopita, lakini habari zake zimewekwa wazi na vyombo vya
dola na waandishi wa habari Jumatatu hii.
Anthony Wagambie, Kamanda Mkuu wa Polisi eneo la Lae
amethibitisha kutokea tukio hilo huku akiwatahadharisha wananchi kuwa macho,
kwani makumi ya wafungwa hao walifanikiwa kutoroka na ni hatari kwa usalama.
Habari zinasema kuwa, tukio
hilo lilifanyika katika gereza la Buimo mjini Lae, ambapo mbali na wafungwa 17
kuuawa kwa kufyatuliwa risasi, wengine zaidi ya 50 walifanikiwa kutoweka.
Mwaka jana, tukio kama hilo lilifanyika nchini humo, ambapo
wafungwa 12 waliuawa, 18 kujeruhiwa huku 94 wakifanikiwa kutoroka jela.
Kituo cha Kurekebisha Tabia cha Buimo chenye uwezo wa
kubeba wafungwa 400, kwa sasa kimefurika wafungwa zaidi ya 1000.
0 comments:
Post a Comment