Wanasayansi nchini
Nethelands wameanza kufanya majaribio ya chanjo ya kupunguza kiwango cha mafuta
mwilini mwa binadamu ambapo kama itafanikiwa kuna matumaini makubwa ya
kupunguza magonjwa ya moyo.
Watafiti hao wamesema kuwa
majaribio yao waliyokwisha kuyafanya dhidi ya panya yanaonesha kwamba chanjo
hiyo imefanikiwa kuzuia na kuacha kuimarisha amana ya mafuta katika mishipa ya
damu
Wamesema kuwa chanjo hiyo
inaweza kutumika kama njia mbadala ya kupunguza na kuwasaidia mamilioni ya watu
ulimwenguni kupambana na mafuta yasiyohitajika mwilini hivyo kupunguza magonjwa
ya moyo.
Hata hivyo, chanjo hiyo
inatarajiwa kuchukua takribani miaka sita ili vipimo hivyo kuanza kufanya kazi
kwa binadamu kwa kutoa tiba ambayo itakuwa ni mkombozi kwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment