Tuesday 20 June 2017

MWANAMUME ALAZIMIKA KUMLIPIA MAHARI MAREHEMU…

Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane, alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikendi iliopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.



Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua, nduguze walimlazimisha mpenziwe kulipa Lobolo, wakionya kwamba la sivyo hatozikwa.
Ndugeze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake, ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo, kabla ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya harusi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Huo ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Mozambique, hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.

0 comments:

Post a Comment