Wanaume wanaochelewa kuanza familia, wana uwezo wa
kupata wavulana werevu kulingana na utafiti.
Watoto hao
huwa werevu na wenye malengo kulingana na utafiti huo, uliofanywa na chuo cha
Kings mjini London.
Umri wa
mama huwa hauna athari yoyote na wasichana huwa na kinga.
Mwanasayansi
mmoja anasema kuwa wanaume wataendelea kuchelewa kuanzisha familia, basi
tunaelekea katika jamii yenye watu werevu mno watakaoweza kusuluhisha matatizo
duniani.
Matokeo ya
utafiti huo ni habari njema katika sayansi ya kuchelewa kuanzisha familia.
Tafiti
zilizorejelewa zimeonyesha kuwa, manii ya mtu mzee hukumbwa na matatizo ya jeni
na kwamba watoto huzaliwa na ugonjwa wa kiakili.
Watafiti
waliwaangazia pacha 15,000 walioshiriki katika utafiti uliokuwa ukichunguza
ukuwaji wao.
Kundi hilo
la watafiti baadaye walichapisha tabia za watoto hao wakati wakiwa na umri wa
miaka 12.
Wale
waliochunguzwa walionekana kufanya vyema shule, hususana katika masomo ya
sayansi, teknolojia, uhandisi na uhasibu.
0 comments:
Post a Comment