Ramadhani Nombo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha
Chang’ombe Temeke jijini Dar es Salaam, kwa kosa la kupenyeza simu tano kwenye
gereza la Keko.
Mtuhumiwa huyo
alikamatwa baada ya chakula alichopeleka gerezani, kutoa mlio wakati wa
ukaguzi.
Kitendo hicho kilitiliwa shaka na askari magereza ambao
walikikagua.
Walipochunguza zaidi waligundua kuwa kwenye chakula hicho,
kulikuwa na simu tano.
Nombo aliweka simu hizo tano zikiwa zimezungushiwa karatasi ya
plastiki nyepesi kuzuia uharibifu, na kuweka katikati ya chakula aina ya ndizi
nyama, ambazo zilikuwa kwenye bakuli kubwa.
Lakini zoezi hilo
halikuweza kufanikiwa baada ya kubainika na kutiwa nguvuni.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam Augustine Mboje, alisema
mtuhumiwa anashikiliwa Kituo cha Polisi Chang’ombe na baada ya mahojiano kwa
kina atapandishwa kizimbani, kwani kitendo alichofanya ni uhalifu kama ulivyo
uhalifu mwingine.
0 comments:
Post a Comment