Wafanyabiashara
ya huduma za usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wametajwa katika
utafiti kuwa wanaowanyanyasa kimapenzi na kuwafanyia ukatili wasichana
wanaokataa kushirikiana nao kimapenzi.
Kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti uliofanywa na shirika
lisilo la kiserikali la Maadili Center na kutolewa jana na Mwenyekiti wa
shirika hilo Florentine Senya, watoto wengi wa kike walitaja kero kubwa kuwa ni
waendesha pikipiki hao (bodaboda) kuwanyanyasa hadi kufikia hatua ya kutishia
kuwagonga kwa pikipiki zao wasichana hao wanapokataa kujihusisha nao kimapenzi.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana kuhusu utafiti wa malezi na maadili ya watoto wa kike uliofanywa na
shirika hilo, Senya alisema utafiti huo unaendelea hadi sasa ulifanywa katika
shule za sekondari na msingi kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Arusha na
Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, utafiti huo pia umebaini
kuwa asilimia 78 ya familia nyingi zina matatizo ikiwemo wazazi kutelekeza
familia zao na kuwaacha wengi kujihudumia wenyewe jambo linalochangia kuwapo
ongezeko la watoto wasio na maadili.
Alisema utafiti umebaini kuwa, watoto wa kike 10 kati
ya 50 sawa na asilimia 20, wamepitia vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo
kupigwa na wazazi, kuchomwa moto wanapokosea, na hata kutishiwa maisha
wanapokataa kujihusisha kimapenzi na watu waliowazidi umri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maadili Center, Rosaline Castillo alitaka
jamii ikubali ukweli kuwa wazazi wengi wametelekeza watoto katika malezi.
0 comments:
Post a Comment