Mji mkuu wa
Angola Luanda, umechukua nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani, kwa
wataalamu na kuusukuma mji wa Hong Kong hadi nafasi ya pili.
Hii imetokana na takwimu za gharama ya kuishi kutoka na
utafiti ulifanywa na shirika la Mercer
Miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi
tano za kwanza.
Mji wa London
ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni.
Utafiti huo wa kila mwaka, huangazia masuala kadha kando na
gharama ya kukodi nyumba.
Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji,
ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.
0 comments:
Post a Comment