Thursday 29 June 2017

HAJI MANARA ATOA POLE KWA RAIS TFF…..

Mara baada ya taarifa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuwashikilia Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake
Mwesigwa Celestine, kwa tuhuma za rushwa leo mapema msemaji mkuu wa klabu ya Simba (aliyesimamishwa), Haji Manara ametoa salamu za pole kwa viongozi hao.

Haji Manara amesema sisi kama wanadamu tunapitia changamoto nyingi sana hivyo ni bora tukafarajiana japo hata kwa kupeana pole pale mwenzio anavyopatwa na matatizo.
“Poleni Viongozi wangu wa TFF,no matter wat!!ni challenges tu ktk life, bnadaam hatufai kuombeana mabaya,hata kama huwakukutendea haki, Mungu awasimamie kutendewa HAKI,“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Haji Manara ambaye alipigwa alisimamishwa kazi na TFF ya kutokujihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja kwa makosa ya kinidhamu bado anaendelea na msimamo wake wa kuitumikia klabu yake ya Simba kama kawaida kwani alilitaka Shirikisho hilo limpe barua ya kumsimamisha.

0 comments:

Post a Comment