Baada ya kutangaza kuachia ngazi kwa kile kilichosemekana
kutokushirikishwa katika maamuzi ya kuingia udhamini kati ya Simba na Kampuni
ya Sportspesa,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe,
ametangaza kutengua maamuzi yake ya kujiuzuru nafasi hiyo na Uenyekiti wa
usajili na kurudi kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Aidha, Hans poppe amefikia maamuzi hayo mara baada ya kufanyika
kwa kikao kilichochukua masaa kadhaa usiku wa kuamkia leo cha kujadili mambo
mbalimbali kuhusiana na uamuzi wa kuingia udhamini na Kampuni hiyo.
Jana Mwenyekiti huyo wa Kamati ya usajili ya Simba alitangaza
kujiondoa kwenye kamati ya utendaji na kubaki mwanachama wa kawaida ili kupisha
kile ambacho alikiita sintofahamu ndani ya Klabu hiyo.
“Kweli tumekutana kikao kilianza mapema lakini tuliendelea
kujadili mambo mbalimbali mpaka mida kama ya saa tisa usiku hivi, ndipo
tulipokubaliana na tumeyamaliza vizuri na sasa tunasonga mbele,”amesema Hans
Poppe.
Simba majuzi ilisaini mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya
Sportspesa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.9 hivyo kusababisha baadhi ya
viongozi kuingiwa na taharuki ya kile kilichotokea
0 comments:
Post a Comment