Thursday 11 May 2017

DALILI HIZI ZINAKUONYESHA KUWA HUNYWI MAJI YA KUTOSHA…

Maji ni muhimu sana katika mwili wa binadamu, yanahitajika kwa zaidi ya asilimia 60 katika mwili.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonesha kuwa idadi ya watu kunywa maji duniani imeongezeka kutoka asilimia 76 mwaka 1990 mpaka kufikia asilimia 91 kwa mwaka 2015.

Niwazi kwamba kiwango cha unywaji wa maji kinatofautiana baina ya mtu na mtu. Aidha inashauriwa kwa siku mtu kunywa zaidi ya lita mbili za maji kiafya kwani binadamu hupoteza maji mengi kwa kutoka jasho na mkojo.
Dar 24 leo inakufahamisha dalili zitakazokuonyesha kiwango chako cha unywaji wa maji, kama unakunywa maji ya kutosha au haunywi maji ya kutosha.
·         Kupungua kwa kiwango cha mkojo
Kiafya mtu anatakiwa kwa wastani akojoe mara 6 hadi saba kwa siku. Kama unakojoa chini ya mara mbili kwa siku basi gundua hunywi maji ya kutosha.
·         Ngozi kuwa kavu sana
Ukiona una ngozi kavu basi tambua huna maji ya kutosha mwilini kwani ata kiwango cha maji kwenye ngozi yako inatokana na unywaji wako wa maji..
·         Kuumwa kichwa
Ukiona unasumbuliwa sana na kichwa basi tambua kichwa hicho kinawezekana kua ni sababu ya upungufu wa maji.
·          Mdomo mkavu
Ukosefu wa mate na mdomo kuwa mkavu hiyo husababishwa na upungufu wa maji.
·          Rangi ya mkojo
Rangi ya mkojo inatakiwa iwe nyeupe ikiwa na unjano kwa mbali kama unakunywa maji ya kutosha. Kama ukiona rangi ya mkojo si ya kawaida kuwa njano kupitiliza basi tambua una upungufu wa maji mwilini.


0 comments:

Post a Comment