Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmark kimetengeneza bia mpya kwa
kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa kutumia lita 50,000 za mkojo.
Kampuni ya Norrebro
Bryghus inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na
masalio yoyote ya mkojo wa binadamu.
Pombe hiyo imepewa
jina Pisner na imeandaliwa kwa kutumia kimea cha pombe kutoka wka shayiri
iliyokuzwa kwa kutumia mkojo huo badala ya mbolea ya kawaida.
Mkojo huo ulikusanywa
kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya
kaskazini miaka miwili iliyopita
"Wakati habari
kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa
tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema
mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus. "Kama ingekuwa na
ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu
moja ambaye alihudhuria tamasha hiyo ya muziki mwaka 2015.,
Lita hizo 50,000 za
mkojo zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa
60,000 za bia.
Kutumia kinyesi au
mkojo wa binadamu kwa kiwango kikubwa hivyo ni jambo ambalo si la kawaida,
baraza la kilimo na chakula nchini Denmark linasema.
Baraza hilo ndilo
lililotoa wazo hilo la kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri
ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe.
Lakini usishangae,
tayari kuna mtambo wenye uwezo wa kubadilisha mkojo moja kwa moja na kuwa bia.
Mashine
iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji,
inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja na mbolea ikitumia
nguvu za miali ya jua.
Maji hayo, kutoka kwa
mkojo uliokusanywa kwa siku kumi katika tamasha moja la muziki Ghent kisha
yalitumiwa kutengeneza bia.
0 comments:
Post a Comment