Monday, 15 May 2017

TCRA YATOA ONYO KUHUSU VIRUSI MTANDAONI…

Kufuatia tishio la kuwapo programu mtumishi (software) yenye virusi aina ya WannaCry, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe zao.

Aidha, taasisi zimetakiwa kutunza data nje ya mtandao ili kuepuka athari endapo kompyuta zitashambuliwa na virusi hivyo, sambamba na kuhuisha mifumo ya ulinzi dhidi ya virusi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alibainisha kuenea kwa programu mtumishi hiyo yenye virusi vinavyoathiri na kumzuia mtumiaji kufikia mafaili au mifumo, ama kwa kufungia mifumo ya screen au kuharibu faili kwenye kompyuta.
“Likitokea tatizo hilo hackers (wadukuzi) wanadai kiasi fulani cha fedha ili kuweza kuzipata faili kwenye kompyuta. Kulipa hizo fedha hakukupi hakikisho la kupata mafaili yaliyoathirika, hivyo tunawashauri watumiaji na taasisi kutolipa fedha.” “Endapo mtumiaji au taasisi wanakumbwa na tatizo hilo basi watoe taarifa kwa Timu ya kitaifa ya dharura ya kompyuta (TZCERT),” alisema.
Kilaba alisema tishio la virusi WannaCry haliko kwenye kompyuta pekee bali pia kwenye simu za kisasa endapo utafungua kiambatanisho au link yenye virusi hivyo.

Kilaba alisema virusi WannaCry kinaharibu programu za kwenye kompyuta zilizopitwa na wakati au software zenye shida hususani Microsoft Server Message Block 1.0 (SMBv1) zilizotolewa mapema mwaka huu na Microsoft kama njia ya kuzuia mazingira magumu na watumiaji wa Microsoft wanaweza kuokoa kompyuta zao kwa kuweka njia za usalama.

Related Posts:

  • CHINA KUZINDUA MTANDAO USIODUKULIWA…. Wakati udukuzi wa mitandao wanapoendesha udukuzi zaidi, China inatarajiwa kuzindua mtandao usiodukuliwa ikimaanisha kuwa itakuwa rahis kugundua kabla ya wadukuzi kuingia. Mradi huo wa kichina katika mji wa Jinan na unau… Read More
  • TCRA YATOA ONYO KUHUSU VIRUSI MTANDAONI… Kufuatia tishio la kuwapo programu mtumishi (software) yenye virusi aina ya WannaCry, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe za… Read More
  • BETRI KUBWA ZAIDI DUNIANI KUUNDWA.. Betri kubwa zaidi ya lithium duniani itaundwa na kuwekwa nchini Australia, kupitia makubaliano kati ya kampuni inayounda magari ya kutumia umeme ya Tesla na kampuni ya kawi ya Australia Neoen. Betri hiyo inatarajiwa kul… Read More
  • SIMU ZA NOKIA 3310 KUREJEA…? Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena baadaye mwezi huu. Kampuni ya HMD Global Oy ya Finland, ambayo ina haki za kuunda bidhaa za nembo ya Nokia ndiyo inayodaiwa k… Read More
  • SAMSUNG YATUMIA SEHEMU ZA NOTE 7 KUUNDA SIMU MPYA….. Kampuni ya mawasiliano ya Samsung imeanza kuuza simu nyingine ambazo inasema imetumia baadhi ya sehemu na vipande vilivyokuwa kwenye simu za Galaxy Note 7 ambazo zilikumbwa na matatizo. Simu hizo za Galaxy Note 7 ziliku… Read More

0 comments:

Post a Comment