Monday 1 May 2017

UKOSEFU WA AJIRA UMETAJWA KUSABABISHA VIFO…….

Utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa moyo kutoka European Society of Cardiology, umetaja ukosefu wa ajira kuwa chanzo cha vifo kwa zaidi ya asilimia 50 ya wanaume hasa wanaougua maradhi ya moyo.


Utafiti huu ulionesha kutoka mwaka 1997 hadi kufikia mwaka 2012, zaidi ya watu elfu 11 mia 8 na 80 ambao ni sawa na asilimia 42, walikufa kutokana na magonjwa ya moyo baada ya kukosa ajira.

Kwa mujibu wa Dr Roerth uhusiano uliopo kati ya ukosefu wa ajira na vifo, unatokana na msongo wa mawazo, watu kujiua na magonjwa ya shinikizo la damu.

Utafiti huo pia ulionesha zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo, vinatokea baada ya mtu kufukuzwa kazi au kukosa kazi.

Pia ugonjwa wa moyo ukionekana kama sababu ya vifo vingi, ukilinganisha na magonjwa kama kisukari na pressure.

0 comments:

Post a Comment