Watafiti
nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na
Amerika ya Kaskazini zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI
wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na virusi.
Wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha
Bristol, waliwachunguza watu wenye virusi vinavyosababisha UKIMWI wapatao elfu
tisini.
Makadirio yao yanaonesha kuwa mtu mwenye umri wa miaka 21
aliyeanza matibabu mwaka 2008 au baadaye anaweza kuishi mpaka kufikia umri wake
wa miaka 70.
Zaidi ya watu milioni mbili
wanaishi na Virusi vya UKIMWI katika Ulaya na Amerika Kaskazini.
Kwa upande wa Takwimu za
ulimwengu, watu walioathirika na virusi hivyo ni milioni 36 wengi wao wakiwa
barani Afrika
0 comments:
Post a Comment