Thursday 17 March 2016

TIBA YA KISUKARI KUTOLEWA BURE…

Serikali itaanza kutoa bure matibabu ya ugonjwa wa kisukari ili wananchi wengi waweze kufikiwa na huduma hiyo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema licha ya serikali kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti, itahakikisha inatoa matibabu hayo.
Akizungumza katika mkutano wa tatu uliowakutanisha wataalamu wa ugonjwa wa kisukari kutoka nchi mbalimbali, kujadili namna ya kupambana na ugonjwa huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigangwala, amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa sera ya Afya inayoitaka wizara hiyo kutoa huduma ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari bure.
Amesema wizara hiyo imekuwa na dhamana katika sera ya afya kutoa tiba bure kwa wagonjwa wa kisukari nchini, ila kutokana na uwezo wa fedha kuwa mdogo wameshindwa kuwajibika katika kutoa tiba stahiki na kusababisha idadi ya wagonjwa kuongezeka.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ugonjwa wa Kisukari (TDA) Profesa Andrea Swai, amesema ugonjwa huo huweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila mhusika kujigundua na husababisha kuharibu, figo, macho pamoja na mishipa ya damu.

0 comments:

Post a Comment