Friday, 11 March 2016

MBUNGE ATIMULIWA BAADA YA KUTINGA NA MKOBA WA KIKE BUNGENI..!!

Spika wa muda wa Bunge la Kenya Tom Kajwang’, amemfukuza mbunge Peter Opondo Kaluma
baada ya kuingia bungeni na mkoba wa kike.

Alimwambia kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo, ni wabunge wanawake tu, wanaoruhusiwa kuingia ukumbini wakiwa na mikoba lakini siyo wanaume.
Kabla ya kuondoka Kaluma alijitetea kwa kusema mkoba aliobeba ulikuwa zawadi aliyopewa na wabunge wanawake, kama zawadi kwa kuwa mtetezi wa haki za wanawake.

Mbunge wa Mbita Mille Odhiambo, amesema mkoba ambao Kaluma alibeba ulikuwa haujaidhinishwa na kanuni za Bunge.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment