Wednesday 23 March 2016

MJAMZITO AJIFUNGULIA MTOTO CHOONI…....

Msichana wa umri wa miaka 17 ambaye alikuwa katika machungu ya uzazi, amejikuta akijifungulia
mtoto chooni baada ya muuguzi mmoja wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, kumtaka aende kuoga na kubadilisha nguo bila ya kujali hali yake.
Msichana huyo Asha Sudi (17) mkazi wa Tabata Kisiwani, alikutwa na tukio hilo juzi wakati akisubiri kujifungua, na uongozi wa Amana umesema utalishughulikia suala hilo.
Asha amesema alifika hospitalini hapo saa 4:00 asubuhi akiwa anaumwa na uchungu, na alipofika mapokezi alikalishwa kwenye benchi.
Amesema akiwa chooni anajiandaa kuoga uchungu ulikata ghafla, na baada ya dakika chache aliona kitu kinaning’inia sehemu za siri kisha kikadondoka chini.
Baada ya kuona hivyo alianza kupiga kelele akiita “nesi nesi” na ndipo alipopita wa kwanza, ambaye hata hivyo hakumshughulikia na badala yake akaendelea na kazi zake, lakini baadaye akaenda daktari ambaye hakumtambua kwa jina akamsaidia.
Baadhi ya wauguzi walitoa ushuhuda wa tukio hilo wakiwamo daktari aliyemuokoa mama huyo na mwanaye chooni, lakini hawakutaka majina yao yatajwe.
Muuguzi mwingine ambaye alikuwa zamu mchana amesema kuwa, alipopita kumuangalia mtoto huyo alikuta akiwa na uvimbe kwenye paji la uso.
Mkuu wa Idara ya Wazazi Grace Massawe amesema wamelichukua suala hilo na kwamba watalishughulikia, lakini akawataka wazazi na ndugu wa mama huyo kuwa watulivu na kuwasamehe waliofanya tukio hilo.

Mkuu wa Idara ya Mama na Mtoto wa hospitali hiyo Francis Kioweli, amesema mtoto huyo hajapata athari ya kiafya na kwamba endapo kutatokea tatizo lolote, basi wazazi hao wasisite kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.

0 comments:

Post a Comment