Thursday 10 March 2016

MWANAMKE AMSAFIRISHA MTOTO NDANI YA BEGI..!!

Shirika la ndege la Air Ufaransa limesema kuwa, mwanamke mmoja alisafiri kwa ndege kutoka Istanbul nchini Uturuki hadi
mjini Paris, akiwa na mtoto aliyemficha katika begi lake la mkononi.
Shirika hilo limesema kuwa mtoto huyo aliyesafiri bila kulipa nauli, alipatikana ndani ya ndege hiyo siku ya Jumatatu usiku.
Duru katika shirika hilo iliambia shirika la habari la AFP kwamba, mwanamke huyo ni mkaazi wa Ufaransa ambaye alikuwa katika harakati za kumfanya mtoto huyo kutoka Haiti kuwa wake.
Shirika hilo la ndege liliwaelezea mamlaka ya Ufaransa, lakini waendesha mashtaka wakaamua kutofungua mashtaka kwa mwana mama huyo.
Mwanamke huyo alikuwa akingoja kuchukua ndege nyengine mjini Istanbul, lakini akazuiliwa kupanda ndege hiyo na mtoto huyo.
Alipokuwa ndani ya ndege hiyo alimuweka mtoto huyo katika miguu na kujifunika na blanketi, lakini mtoto huyo wa kike alitaka kwenda chooni na alionekana na abiria wengine.

Haijulikani mtoto huyo alikuwa na miaka mingapi, duru moja ilieleza kwamba alikuwa na miaka minne huku nyengine ikisema alikuwa na mwka mmoja ama miwili.

0 comments:

Post a Comment