Povu
linalotengenezwa na vyura wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao, linaweza
kuponya majeraha ya wagonjwa walioungua wamesema wanasayansi.
Povu gumu linaweza kukusanywa na
kutumiwa katika mchakato wa matibabu, kama kizuizi baina ya bandeji na ngozi
iliyoungua wanaamini.
Watafiti katika Chuo kikuu cha
Strath clyde, wameanza majaribio ya sehemu ya povu hilo.
Wanafanya majaribio hao kwa kutumia povu kutoka kwa vyura
hao wadogo, kutoka kisiwa cha Tungara huko Trinidad.
Vyura hao kutoa povu lenye urefu
wa sentimeta 5,ili kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa
wastani wa siku tano.
Imeelezwa kuwa povu hilo limetengenezwa kwa aina tano za
Protini.
Doctor Paul Hoskisson na wenzake
wanasema kuwa, wameweza kuzichunguza aina nne za protini hizo na wameanza
kuzichanganya na dawa zao.
Watafiti hao watawasilisha kazi
yao katika katika mkutano wa mwaka, wa kituo cha uratibu wa shughuli za utafiti
wa viumbe hai Microbiology Society, utakaofanyika Liverpool.
0 comments:
Post a Comment