Wednesday, 2 March 2016

HIZI NI NCHI ZINAZOONGOZA KWA RUSHWA NA UFISADI DUNIANI….!!

Nchi tatu za Afrika zimetajwa kwenye orodha ya nchi tano zilizokithiri kwa vitendo vya rushwa
duniani katika ripoti ya Shirika la kimataifa Transparence iliyotolewa hivi karibuni.
Miongoni mwa nchi tano zinazoongoza mataifa ya Bara la Afrika, Somalia, Sudan na Sudan Kusini yametajwa.
Somalia ndiyo taifa linaloongoza kwa ufisadi kwa kushika nafasi ya 167 ikifungana na Korea Kaskazini, Sudan Kusini likishika nafasi ya 163 kwa kufungana na Angola, Sudan ikiwa nafasi ya 165.
Nchi nyingine iliyo katika nafasi tano za juu kwa rushwa na ufisadi duniani ni Afghanistan iliyo na alama 166.
Katika ukanda ya Afrika Mashariki, Burundi inaongoza kwa kiwango cha juu cha rushwa na ufisadi ikiorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa kupata jumla ya alama 21.
Uganda na Kenya zimefungana katika nafasi ya 139 zikiwa na alama 25 huku Tanzania ikiwa katika nafasi ya 117 duniani kwa kupata alama 30.
Mwaka 2012 Tanzania ilishika nafasi ya 102 kwa rushwa duniani kati ya nchi 174 baada ya kupata alama 35.
Mwaka 2013, ilikuwa ya nchi ya 111 kwa alama 33, mwaka 2014 ikaporomoka hadi nafasi ya 119 baada ya kupata jumla ya alama31.
Swali linalobaki ni kwamba chini ya uongozi wa Rais Magufuli rushwa itaendelea kukithiri Tanzania au itapungua na kuthibitiwa?
Wakati Burundi ikitajwa kuongoza kwa rushwa Afrika Mashariki, Rwanda imetajwa ni taifa linaoongoza kwa kupiga vita ufisadi, ikiwa na alama 54 na kushika nafasi ya 44 kidunia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo nchi tano zenye kiwango kidogo cha rushwa na ufisadi duniani zinaongozwa na Denmark inayofuatiwa na Finland, Sweden ikiwa ya tatu, New Zealand na Uswisi imeshika nafasi ya tano.

0 comments:

Post a Comment