Mother Teresa alikuwa mtawa wa kanisa Katoliki Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu. |
Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.
Njia ya kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
Alizaliwa 1910 eneo ambalo kwa sasa hujulikana kama Macedonia na wazazi wa asili ya Albania na kupewa jina Agnes Gonxha Bojaxhiu.
Alipewa uraia kamili wa India baada ya kuanzisha kikundi cha watawa cha Missionaries of Charity mwaka 1950.
Alifariki 1997 akiwa na umri wa miaka 87 na alifanywa mbarikiwa mwaka 2003.
0 comments:
Post a Comment