Serikali ya Marekani imeamua kutaifisha mali za
mfanyabiashara wa dawa zilizopigwa marufuku za kulevya kutoka Tanzania Ali
Khatib Haji Hassan maarufu kwa jina la Shikuba.
Wizara
ya fedha nchini Marekani imemtaja raia mmoja wa Tanzania Ali Khatib Haji Hassan
na mtandao wake, kama kinara wa usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kushiriki
katika usafirishaji wa kimataifa wa dawa za kulevya.
Kwa
hatua hiyo marekani ilimuwekea vikwazo Hassan na jamaa wanaohusika naye kwenye
harakati hizo, na kupoteza sifa ya kupata Viza ya kuingia Marekani.
Taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani mjini Washington hapo Jumatano
ilisema kuwa, Hassan alikuwa akihusika katika usafirishaji wa shehena kubwa za
dawa za kulevya kwenda mataifa ya Afrika, ulaya, Asia na Marekani.
Hassan
alikamatwa na serikali ya Tanzania mwaka 2014, kwa kujaribu kuingiza kiasi cha
kilogram 210 za dawa aina ya heroin mwaka 2012.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania bibi Virginia Blaser, amesema katika taarifa yake kuwa Marekani imefurahi kushirikiana kwa karibu na Tanzania, katika kudhibiti vitisho vinavyotokana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kama Hassan na mitandao ya kihalifu inayowasaidia.ra wa dawa za kulevya kama Hassan na mitandao ya kihalifu inayowasaidia
Kiwale 11 Blog imemnasa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga, na kwanza anaeleza
iwapo serikali ya Tanzania inafahamu lolote kuhusiana na swala hilo.
0 comments:
Post a Comment