Wednesday 30 March 2016

WHO: EBOLA SIO TISHIO TENA KWA DUNIA…

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa, maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi sio tena kitisho cha dunia.

Mkurugenzi wa shirika hilo Margaret Chan ametangaza kumalizika kwa kipindi cha dharura cha miezi 20, ambapo kiasi ya watu elfu 11 na 300 walikufa kutokana na ugonjwa huo, wengi wao wakiwa kutoka Afrika.
Hata hivyo wataalamu wa WHO walionya kuwa, virusi vya Ebola vinaweza kuishi kwa muda mrefu kwenye mbegu za kiume za baadhi ya wanaume walionusurika, hivyo kuna hatari ya ugonjwa huo kuambukizwa kwa njia ya ngono.

Chan ametoa wito wa juhudi zaidi za kutafutwa chanjo ya Ebola, na kuwepo vipimo bora vya uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment