Wednesday 9 March 2016

ALIYEWANG'OA MENO WATU 100 ASHTAKIWA UFARANSA..!!

Daktari moja wa meno mholanzi, ameshtakiwa nchini Ufaransa kwa kuwakata midomo zaidi ya wateja wake 100 maksudi.

Daktari huyo anayefahamika kwa majina kamili ya Jacobus van Nierop, anakabiliwa na mashtaka ya kung'oa meno yenye afya kwa kisingizio tu wateja wake.
Nierop anasemekana kuwajeruhi vibaya wagonjwa wake, katika kliniki yake iliyoko katika kijiji kimoja huko nchini Ufaransa.
Baadhi ya wagonjwa wake walishikwa na maradhi ya ufizi yaliyosababisha midomo yao kuoza, huku wengine wakiambukizwa maradhi mbali mbali midomoni mwao.
Mahakama iliambiwa kuwa mwanamke mmoja aliyekwenda katika zahanti hiyo, akitaka meno yake yanyooshwe nusura abakie kibogoyo.
Amesema aliibuka kutoka usingizini na kugundua kuwa daktari huyo alikuwa amemng'oa meno 8 abayo hayakuwa na matatizo!
Hata hivyo Daktari huyo alitorokea nchini Canada, alipogundua anatafutwa na maafisa wa polisi.
Lakini alipatikana na sasa amerejeshwa nchini Ufaransa alikotekeleza unyama huo ili haki itendeke.
Endapo atapatikana na hatia Daktari Jacobus van Nierop, huenda akafungwa jela kwa miaka 10.

0 comments:

Post a Comment