Thursday 10 March 2016

JUA LANASWA NA MWEZI INDONESIA…

Raia Indonesia wameshuhudia jua likizibwa kikamilifu na mwezi.ikiwa ndio nchi pekee iliyoshuhudia tukio hilo kote duniani.

Hoteli zilizopo katika maeneo mazuri ya kushuhudiwa jua likinaswa zilijaa miezi kadhaa iliopita, na katika baadhi ya maeneo ilibidi maafisa watafute nafasi za ziada kwa watalii waliokuwa kwenye maboti.
Katika kisiwa cha Belitung mamia ya wageni na watalii nchini humo, walikusanyika katika fukwe za bahari kabla ya alfajiri.
Wakati jua lilipoanza kunaswa na mwezi walishangilia, na baadaye kunyamaza kimya kwa mshangao wengi wakilielezea tukio hilo kama tukio la miujiza.
Kwa wengi nchini humo tukio hilo linashirikishwa sana na dini na watu huomba, sherehe za kitamaduni na ngoma zimeandaliwa katika sehemu kubwa la eneo hilo.

Wanasayansi pia wamekuwepo hususan katika eneo la Maba katika visiwa vya Maluku, ambako tukio hilo limeshuhudiwa kwa dakika tatu, ambao ni muda mrefu kuwahi kushuhudiwa jua likinaswa na mwezi.

0 comments:

Post a Comment