Tuesday, 1 March 2016

RUFANI YA BABU SEYA KUSIKILIZWA MACHI 11..!

Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) katika kikao chake kilichoanza jijini Arusha,
itapitia maombi ya rufani ya mwanamuziki maarufu nchini Nguza Viking na John Viking dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo jana, ilieleza kuwa kesi hiyo namba 006/2015 iliyopangwa kusikilizwa Machi 11   haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.
Ni kesi mbili pekee kati ya 50 zitakazosikilizwa kwenye mahakama ya wazi, ikiwamo inayomhusu mwanasiasa maarufu wa Rwanda Victoire Ingabire, aliyoifungua kupinga ukiukwaji wa haki anaofanyiwa na Serikali yake.

Pia mahakama ilieleza kuwa kikao hicho cha 40 cha kawaida, kitakamilika Machi 18 na kutoa uamuzi wa mashauri manne.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment