Shirika la
ufadhili la serikali ya Marekani, limesitisha msaada wake kwa serikali ya
Tanzania
likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa
Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC),imesema
Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka
kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao
ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja
za Tanzania.
Kupitia taarifa bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania
haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa
kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”
Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa
marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya
wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya
kimataifa.”
Mgombea urais
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa
uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).
MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na
kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.
"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria
ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.
Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.
Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na
nishati.
Source:BBC swahili
0 comments:
Post a Comment