Monday, 21 March 2016

DR SHEIN ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS ZANZIBAR…

Uchaguzi wa marudio Zanzibar jana, ulifanyika katika hali ya utulivu tofauti na baadhi ya watu walivyokuwa wakifikiria.


Hali ya amani na utulivu ilitanda kuliko uchaguzi wowote uliofanyika tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, huku baadhi ya watu wakisifu hali hiyo.

Dr Ali Mohamed Shein ametangazwa mshindi kwa kupata asilimia 91 ya kura zote halali zilizopigwa, katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana Machi 20 2016.

Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura elfu 6 na 76 kwenye uchaguzi huo wa marudio uliofanyika jana

Hamad Rashid Mohamed wa chama cha ADC, ndiye aliyemfuatia Dr Shein kwa wingi wa kura kwa kujipatia kura elfu 9 mia 7 na 34.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment