Dubai
imepiga marufuku wanawake waja wazito, kuvuta ama hata kuingia katika migahawa
inayouza Shisha.
Hatua hiyo inafuatia shinikizo la
kuimarisha afya ya umma na haswa afya ya mama waja wazito.
Sheria hiyo inawadia baada ya
kampeini ya kuwazuia wanawake wajawazito kuingia pahala panapovutiwa sigara
jarida la Gulf News limesema.
Kampeini hiyo inayoendeshwa kwa
kutumia mabango na picha ya mwanamke mjamzito akiambiwa na mwanaye aliyeko
tumboni kuwa ''Uamuzi wa kuvata au la ni wako sio wangu''
Mabango hayo yanaeleza kuwa
watoto ambao hawajahitimu miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta
shisha au sigara.
Mkurugenzi wa afya ya umma wa Dubai bwana Marwan Al
Mohammed,amesema kauli hiyo ni ya serikali wala sio hoja ya kujadiliwa na mtu yeyote.
Wamiliki wa vilabu vya burudani
vinavyouza shisha, wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa sheria zinazoharamisha
wanawake wajawazito kutoingia katika vilabu hivyo.
Mwaka wa 2014 milki hiyo ya
kiarabu ilipitisha sheria kali dhidi ya uvutaji wa sigara, ambayo ilipiga
marufuku matangazo ya aina yeyote ya kibiashara ya Sigara.
Vilevile sheria hiyo ilipiga marufuku uvutaji wa sigara
ndani ya gari, iwapo mna mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 12.
Aidha sasa kuna sheria inayotoa
mwelekeo ya ni wapi shisha itauzwa, na itaruhusiwa kuwepo umbali gani kutoka
kwenye makazi ya watu.
0 comments:
Post a Comment