Tuesday 22 March 2016

HUYU NI PAKA MWIZI WA NGUO ZA NDANI ZA WANAUME…!!

Paka mmoja mwizi wakati wa usiku, amekuwa akiiba soksi pamoja na nguo za ndani nchini New Zealand.

Katika kipindi cha miezi miwili paka huyo mwenye umri wa miaka sita kwa jina Brigit kutoka mji wa Hamilton, aliiba bukta za ndani (boxer) 11 na zaidi ya soksi 50.
Mmiliki wake Sarah Nathan alichapisha tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida, katika mtandao wake wa facebook.
Aliandika Lazima kuna mtu ambaye anakosa vitu vyake'', alisema katika chapisho lake la ukursa wa facebook lililosambazwa mara 500.
Bi Nathan ameimbia BBC kwamba tatizo lilianza alipogundua vipande kadhaa vya nguo za ndani, katika nguo zake anapoziosha.
Amesema Bukta hizo za ndani hazikuwa zao,na siku moja Brigit aliingia katika chumba cha wageni akiwa amebeba soksi na ndipo alipogundua kuwa ndiye anahusika kuzileta nyumbani kwako.

Ameongeza kuwa waathiriwa wa paka huyo Brigit, walikuwa majirani katika nyumba za ghorofa.

0 comments:

Post a Comment